DA'ANGW
Nyimbo za wairaqw
Jamii ya Wairaqw huishi kaskazini katikati mwa Tanzania katika nyanda za juu za ziwa Manyara na ziwa Eyasi. Idadi yao ni takribani nusu milioni na huzungumza kikushitiki. Majirani zao huzungumza lugha tofauti kabisa na wao: Wambugwe na Wanyiramba huongea lugha za Kibantu, Wadatooga huongea Kinailotiki na Wahadzabe huzungumza lugha za kubofya isiyoainishwa. Eneo hilo pia lina shughuli mbalimbali za kiuchumi. Jamii ya Kiiraqw ni wakulima na wafugaji kama walivyo Wambugwe, Wadatooga na Wamasai ambao ni wafugaji wakati Wahadzabe ni wawindaji wa asili na huchuma vyakula. Kwa karne sasa hizi tamaduni zimekuwa zikiathiriana wakati huo kila moja akilinda ubora wa tamaduni zake.
Nyimbo katika Jamii
Nyimbo ni sehemu ya maisha ya Wairaqw katika mazingira mbalimbali. Katika vilabu hukosi kusikia nyimbo. Nyimbo mpya hutungwa kuweka kumbukizi ya matukio yaliyopo na yaliyopita. Nyimbo ni chombo muhimu cha kutunza historia ya Wairaqw. Nyimbo huelezea matukio, mambo ya asili kama ilivyo kwenye wimbo namba saba au matukio ya kihistoria, makubwa kwa madogo, kama ilivyo kwenye wimbo namba moja na kumi. Lakini nyimbo hazielezei matukio kwa ufasaha. Mistari isiyohusiana hufanya rejea kwenye matukio kama ilivyo kwa majina. Watu pia hukumbukwa kwa matukio kama jinsi ambavyo wao pia hukumbukwa. Matokeo yake mistari hurudiwa au huimbwa kwa mpangilio tofauti.
Nyumbani utasikia wanawake wakiimba, kwa mfano kipindi wakisaga mtama kwa kutumia jiwe la kusagia. Shughuli katika maeneo mbalimbali huchochewa kwa nyimbo (wimbo 3 na 4) na kazi zingine ngumu za jumuiya kama vile kubeba mawe mazito ya kusaga nyumbani. Baada ya kazi ngumu, watu husherekea kazi nzuri iliyofanyika. Katika matukio haya michezo yote ya kiutamaduni yanaweza kufurahiwa. Shairi maarufu yakuvutia iitwayo slufay huimbwa (Beck & Mous 2014). Au washairi watashiriki dua ya girayda iliyoboreshwa ambapo baadaye wanawake huimba /ayla au sibeli (song 9) ambayo inamuundo ulioboreshwa wenye mpokezano baina ya waimbaji na hadhira. Kwenye sherehe, hususan harusi (wimbo 5), watu hucheza rumba. Wanaume na fimbo zao wakati wanawake huruka mbele kwa mistari au hutengeneza duara. Katika ushairi, nyimbo, na rumba kuna zile ambazo ni mahususi kwa wanaume na zingine kwa wanawake lakini hili halizuii jinsia zingine kushiriki.
Mziki wa Wairaqw
Wakati wa sherehe kubwa kunawepo midundo. Wasichana wadogo hucheza ngoma. Wao hufanya hivyo kwa kuchuchumaa na kuweka ngoma zao chini. Huvuta sketi zao za ngozi kwenye magoti na kuanza kupiga ngoma kwa kutumia kifimbo maalum ili kuzalisha midundo. Kiasili hakuna aina nyingine za ngoma za asili. Watu hutumia makofi na bangili kwa mdundo. Ni dhahiri kuwa zama za kisasa zimeleta alama mpya za mziki zinazotumika kanisani. Waimbaji maarufu hutumia seze kutengeneza nyimbo zao na Safari Ingi ametengeneza CD yake ya namna hii (http://www.andreakt.no/safari-ingi).
Pamoja na nyimbo zilizopangiliwa kidogo au sana kuna tanzu za uimbaji zilizoboreshwa. Nyimbo zenye mpangilio maalum haina taratibu ngumu katika nyanja kama za mpangilio wa mistari. Kila wimbo unamwitikio wake baada ya kila mstari ambayo kwa namna moja au nyingine ni sauti nzuri za silabi ambazo haziwakilishi maneno katika lugha, kwa mfano hiyohayohee. Chakushangaza, sauti hizi hutofautiana wimbo hadi wimbo. Kwa hiyo, kwa kuimba kibwagizo watu huelewa wimbo unamaanisha nini, sauti yake na mdundo. Hivyo, wimbo unaweza kuainishwa baada ya kuimba kibwagizo. Hakuna njia nyingine ya kitamaduni ya kuainisha nyimbo. Mfumo huohuo hutumika katika nyimbo zilizoboreshwa. Mfumo huu ndiyo unaotumika pia katika Sanaa mbalimbali za sauti katika jamii ya kiiraqw. Nyimbo zisizo na kibwagizo hutumika katika hadithi vile vile. Hadithi mbalimbali za kale huwa na nyimbo fupi moja au mbili na nyimbo hizi wakati mwingine huwa na mistari miwili au mitatu yenye maneno ya kustaabisha yasiyo na maana. Nyimbo za watoto na zile nyimbo tulivu hazina kibwagizo vile vile.
Nyimbo za CD
|